Mienendo ya Soko

Uhamasishaji wa Watumiaji Kuhusu Faida za Usafiri wa Umeme

2025-05-10 06:19:37 admin 0
  •  Utafiti wa hivi karibuni ulionyesha kuwa 4 kati ya 10 ya wakazi wa mijini hawajawahi kupanda au kutumia gari la umeme,hasa kutokana na kutoelewa faida zake.

  •  Hili limesababisha baadhi ya mashirika kama TAREA(Tanzania Renewable Energy Association)na kampuni binafsi kuandaa kampeni za elimu kupitia redio,TV na mitandao ya kijamii,zikilenga kueleza kuwa usafiri wa umeme ni wa gharama nafuu,hauna uchafuzi,na unafaa kwa matumizi ya kila siku.

  •  Zaidi ya hayo,maonyesho ya mitaani(roadshows)na majaribio ya bure ya bajaji yameongeza uaminifu kwa bidhaa hizi.Kadri watumiaji wanavyopata taarifa sahihi,ndivyo soko linavyozidi kukua.